Saturday, December 15, 2012

KOFFI OLOMIDE AFUNIKA VIWANJA VYA LEADERS USIKU WA KUAMKIA LEO...

  
Hakika palikuwa hapakaliki katika Viwanja vya Leaders Club usiku wa kuamkia leo pale Gwiji la Muziki wa Dansi kutoka nchini Congo DRC, Koffi Olomide na vijana wake wa bendi ya Quartier Latin walipofanya shoo kali ya 'kufa mtu'. Leo Koffi atashusha burudani kali jijini Mwanza. Video zaidi za shoo za wikiendi utazipata Jumatatu.

Monday, December 10, 2012

TUMERUDI TENA: DANSI MWANZO MWISHO...

   HAKIKA HII SI YA KUKOSA!!!   
Baada ya kimya kirefu, sasa blogu yako makini ya BONGOMOTO inarejea kivingine kwa kishindo wikiendi ijayo Desemba 15, 2012 kwa kukuletea mambo motomoto yanayojiri kwenye kumbi mbalimbali, video kali za shoo LIVE na mengi usiyoyajua kuhusu wanamuziki wa dansi hapa nchini kwenye mahojiano EXCLUSIVE! Kama haitoshi, mpenzi msomaji wa blogu hii sasa utaweza kujishindia zawadi kemkem kila wiki kwa kujibu maswali kadhaa. **Kumbuka hii ni kwa wale tu watakaokuwa wamejisajili kwenye blogu hii** Kaa tayari na hakikisha hukosi burudani hii hapahapa. -Mhariri

Monday, April 2, 2012

SHENGEN ACADEMY WAKIONESHA UMAHIRI WAO JUKWAANI MANGO GARDEN JUZI USIKU...

Wanamuziki wa bendi ya Shengen Academy wakati wa onesho lao kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni juzi usiku. Ni bendi inayotishia amani ya bendi kongwe hakika. (Video ya ziro99blog).

BENDI YA SHENGEN ACADEMY IKISHAMBULIA NDANI YA MANGO GARDEN USIKU WA KUAMKIA JANA...

Wanamuziki wa bendi ya Shengen Academy wakishambulia jukwaa kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni usiku wa kuamkia jana Jumapili. Hawavumi lakini wamo. Ni jina geni kidogo lakini limesheheni wanamuziki wenye majina makubwa katika medani ya muziki. Bendi hii iko chini ya uongozi wa Rais Liva Hassan Sultan. (Video ya ziro99blog).

WANENGUAJI WA AKUDO IMPACT WAKIFANYA KUFURU KWENYE BONANZA...

Wanenguaji wa bendi ya Akudo Impact wakishambulia jukwaa kwa mtindo wa Pekecha-Pekecha! Ilikuwa balaa...Kama ulikosa shoo hii kwenye bonanza la usiku wa kuamkia leo, basi usikate tamaa. Nafasi yako nyingine ni pale Mango Garden, Kinondoni siku ya Ijumaa Kuu na pia Siku ya Pasaka kwenye Bonanza la aina yake maalumu kwa wapenzi wa kupekecha pale Msasani Beach Club. (Video ya ziro99blog).